Ikiwa zimepita siku kadhaa tangu Rais John Magufuli alipokamilisha safu yake ya uongozi wa kuwateua makatibu tawala wa wilaya, mteule katika Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma hajaripoti.
Makatibu tawala hao waliteuliwa katika kipindi ambacho kulikuwa na vuguvugu la uteuzi wa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa wilaya, halmashauri, manispaa na majiji na ilishuhudiwa baadhi yao majina yakijirudia katika uteuzi wa nafasi moja.
Jina la Kasilida Mgeni Mnimila, lilionekana kuwa miongoni mwa wateule wa nafasi ya katibu tawala wa Wilaya ya Bahi, lakini hadi jana kiongozi huyo hakuwa ameripoti kazini.
Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Elizabeth Kitundu alisema walishawasiliana naye na alimwambia kuwa hataripoti

Chanzo: Mwananchi