AUDIO: Kiama cha wanaojichukulia sheria mkononi chatangazwa na DC wa Makete

Wananchi wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi, kwani kwa kufanya hivyo kunaleta athari kubwa kwa jamii Ikiwemo kukatisha uhai wa watu ambao wengi wao ni tegemezi katika maeneo yao na taifa kwa ujumla

Akizungumza kwenye baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete hivi karibuni, Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kesi amesema masuala ya kujichukulia sheria mkononi hayana nafasi hivyo kuagiza endapo linatokea tatizo viongozi husika wajulishwe mara moja ili sheria ichukue mkondo wake, lakini pia akakemea suala la unywaji pombe kupindukia muda wowote bila kujali sheria zinasema nini

Aidha mkuu huyo wa wilaya ameagiza kuanzia sasa viongozi wa vijiji mpaka ngazi ya wilaya kutenga siku maalumu kwa ajili ya wananchi kufika na kutoa kero zao na zitatuliwe mapema iwezekanavyo

Akitoa neno la shukrani kwa maagizo hayo ya Mkuu wa wilaya, Diwani wa kata ya Kipagalo Mh Reuben Mwandilava amesema madiwani wa halmashauri ya Makete wanamuunga mkono katika utekelezaji wa majukumu yake kama mkuu wa wilaya na kuongeza kuwa maagizo aliyoyatoa watayasimamia na kuhakikisha yanatekelezeka
SIKILIZA SAUTI HIZI HAPA CHINI


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo