Aliyegoma kula miaka 16 jela aachiwa

Mwanaharakati nchini India, Irom Sharmila (44) amesitisha mgomo wa miaka 16 wa kula akipinga sheria tata. Alianza mgomo huo Novemba 2, 2000.

Mwanaharakati huyo alianza kula jana baada ya Mahakama ya Jimbo la Manipur Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo kumwachia kwa dhamana.

Aliachiwa akitokea hospitali baada ya taratibu za dhamana kukamilika na mara tu baada ya kutoka, alionja asali mbele ya waandishi wa habari ikiwa ni ishara ya kumaliza mgomo wake.

“Ninataka kula chakula kizuri, ninataka kuolewa, ninataka kupata watoto, tafadhali msinishikilie. Mimi ni mtu wa kawaida ambaye ameshiriki katika mapambano yasiyo ya kawaida,”


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo