Wananchi wa kijiji cha Utweve kata ya Ukwama wilayani Makete mkoani Njombe wameendelea kutekeleza kwa vitendo makubaliano yao na Mkuu wa wilaya ya Makete kuwa wataendelea na shughuli za kimaendeleo kama kawaida wakati kero zao zikiendelea kufanyiwa kazi na serikali
Kufuatia mkutano wao na Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessi hivi karibuni kijijini hapo, wananchi hao walimweleza mkuu huyo kero waliyonayo iliyopelekea wao kugomea shughuli za maendeleo na baada ya mkuu huyo kutoa kauli ya kushughulikia kero zao, wananchi hao walimuunga mkono na kukubali kushiriki shughuli zote za maendeleo kijijini hapo wakati wakisubiri serikali izitatue na kuwapa majibu
Akizungumza na blog hii kuhusu utekelezaji wa shughuli za maendeleo kijijini hapo, Mwenyekiti wa kijiji cha Utweve Bw. Lauten Enock Sanga amesema tayari wamekaa vikao na kukubaliana wananchi kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa zahanati kijijini hapo
Amesema baada ya kukaa kikao hicho wamekubaliana kila mwananchi kuchangia shilingi 7,000/= kwa ajili ya kufyatulia tofali za ujenzi wa zahanati hiyo, ambapo ukusanyaji wa fedha hizo unatarajiwa kuanza August 1 Mwaka huu
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa mbali na kazi hiyo ya ujenzi wa zahanati pia kazi nyingine ya maendeleo kijijini hapo wanayokusudia kuifanya ni ya kuandaa eneo kwa ajili ya kupanda miti kibiashara, ambapo wiki hii wanatarajia kwenda kutembelea eneo lililopendekezwa kwa kazi hiyo kwa ajili ya kulifanyia maandalizi
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amekanusha taarifa zilizoripotiwa na gazeti moja la kila siku hapa nchini kuwa wananchi wa kijiji hicho wamegomea shughuli za maendeleo mbele ya Mkuu wa wilaya, na kusema taarifa hizo sio za kweli na badala yake amesema baada ya wananchi kumueleza mkuu wa wilaya kero ya mauaji yaliyotokea kijijini hapo, na yeye kuahidi kushughulikia suala hilo kwa kufuata sheria za nchi, wananchi wameridhika na majibu yake
Amesema kwa sasa wananchi wanaendelea na shughuli za maendeleo kama kawaida wakati wakisubiri serikali kwa kushirikiana na mamlaka nyingine kulishughulikia suala hilo
Julai 4 mwaka huu katika mkutano wa hadhara kijijini hapo wananchi waligoma kufanya shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati mpaka waonane na Mkuu wa wilaya wamueleze kero zao, jambo ambalo limetekelezwa kwa mkuu huyo kufika na kuwasikiliza

sikiliza sauti hapa chini