Breaking News: Ajali Mbaya ya UDA na Treni Kariakoo Usiku huu, Angalia Picha

Taarifa zilizotufikia usiku huu ni kwamba Basi la UDA limegonga Treni eneo la Kariakoo jijini DSM, kama inavyoonekana kwenye picha, Ajali imetokea usiku huu kati ya treni na basi la Uda linalofanya safari zake kati ya Kariakoo na Mbagala na kuua mtu mmoja na wengine zaidi ya 45 kujeruhiwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Ernest Matiku amesema majeruhi wamepelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.

Hata hivyo, hakuweza kumtaja jina mtu huyo aliyefariki dunia.

“Ni kweli ajali imetokea kuna kifo cha mtu mmoja na watu wengi wameumia sana na hivi ninavyozungumza na wewe naelekea Muhimbili,” amesema Kaimu kamanda huyo., Picha za tukio hilo hizi hapa chini






JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo