Sikiliza hii, Binti aelezea alivyofanyiwa ubakaji na kisha kurekodiwa Video

Tukio la msichana mmoja wa Dumila mkoani Morogoro mwenye umri wa miaka 21 kubakwa na kisha kurekodiwa kwenye simu na video yake kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii limechukua sura mpya kufuatia binti huyo, mama yake mzazi na watetezi wa haki za binadamu kutengwa na jamii huku wengine kutishiwa maisha na watu wasiowafahamu.

Licha ya tukio hilo kuangaliwa kwa sura hiyo lakini pia baadhi ya wanasiasa wamedaiwa kulihusisha na masuala ya kisiasa bila kuangalia uzito wa tukio lenyewe lilivyotokea.

Waandishi wa habari wamefika katika kijiji cha Wami Dakawa na kuzungumza na msichana huyo ambaye jina lake limehifadhiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mama wa binti huyo ambaye amesema tukio hilo linamnyima hata wateja wa biashara yake huku akiishi kwa hofu ya usalama wa maisha yake.

Mwenyekiti wa kijiji cha Wami Dakawa Bwana Abdalah Mgaya amesema serikali ya kijiji inalishughulikia suala hilo kwa kina ili kuhakikisha usalama wa wananchi wake unaimarishwa kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.

Naye mwenye nyumba ya kulala wageni ambapo lilitokea tukio hilo Bwana Levoi Saimon alipotafutwa na waandishi wa habari ili kuzungumzia tukio hilo amekiri kuwafahamu watuhumiwa kama wateja wake kwa takribani mwezi mmoja na kwamba walikuja kijijini hapo wakiwa na trekta kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo na baadaye kuondoka.

Bwana Gabriel Ngoina na Bi Magreth Mwampepo ni wasaidizi wa kisheria wilayani Mvomero ambao wameitaka jamii kuelewa kuwa kuibuliwa kwa suala hilo ni kutokana na kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii na kwamba tayari lipo mikononi mwa serikali


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo