Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Ahmed
Msangi amesema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 22 mwaka huu majira ya
saa 2 usiku.
Msangi
amesema kuwa marehemu aliekuwa akifahamika kwa jina maarufu "msukuma"
mfanyabiashara na mkazi wa bulale aliuawa kwa kupigwa risasi kifuani na
kutokea chini ya kwapa upande wa kulia na watu wawili wasio fahamika
pamoja na risasi hiyo kumjeruhi Neema Marangula (23) Mkazi wa Bulale
katika Kiganja cha mkono wa kulia.
Amesema
kuwa wakati Mwenyekiti huyo akitoka kwenye kikao alichofanya na
wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mtaa wa Bulale akiongozana na
wajumbe wawili alikutana na Neema Marangula akiwa na mume wake ambao
walikua wanawafuata marehemu na Balozi kwa ajili ya kuzungumzia mzozo wa
ndani ya ndoa yao kwa hiyo walikua wanahitaji kusuluhishwa.
Mwenyekiti
huyo (marehemu) na wajumbe wake wawili wakiwa pamoja na Neema pamoja na
mumewe wakiwa wanajadili tatizo hilo hapo barabarani mara ghafla
wakatokea watu wawili ambao walikua wakipita barabarani na kuwaambia mko
chini ya ulinzi na mmoja wao akatoa bunduki na kumpiga risasi
mwenyekiti huyo ambaye alianguka chini huku wenzake wakikimbia kujiokoa
kutoka eneo hilo lakini pia wale wahalifu wakakimbia na kutokomea
gizani vichakani.
Amesema
wananchi wa eneo hilo ambapo mwenyekiti aliuawa walijitokeza kwa
msaada wa kumsaidia walimchukua na kumkimbiza hospitali kwa matibabu
lakini alifariki dunia wakiwa njiani. majeruhi Neema Marangula amelazwa
Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure kwa matibabu na hali yake
inaendelea vizuri.
Mwili
wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali Mkoa wa Mwanza Sekou Toure
kwa ajili ya uchunguzi wa daktari, chanzo cha mauaji hayo bado
hakijafahamika pamoja na uchunguzi tukio hilo bado unaendelea.
Msangi
amewaomba wananchi wenye taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo
zitakazo saidia kufanikisha kukamata wahusika wazitoe polisi lakini pia
kutoa ushirikiano kwa viongozi wao na kuhakikisha wanatengeneza makazi
salama huko wanapoishi na maeneo ya shughuli zao na msako mkali
unafanyika na kuhakikisha wahusika wa tukio hilo wanakamatwa.