Wananchi wa kijiji cha Ikonda kata ya Tandala wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kulifanya Suala la usafi kuwa ni tabia ya kila siku kupitia kaya zao.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa mtendaji wa kijiji cha Ikonda Bw, Raphael Tweve alipokuwa akizungumza katika mkutano wa kijiji uliofanyika katika ofisi za kijiji hicho hivi karibuni.
Pia mtendaji Tweve amesema wananchi wanatakiwa kujiridhisha na wageni waingiapo Kijijini hapo ili kujiepusha na vitendo vya kihalifu.
Kwa upande mwingine afisa mtendaji amewakumbusha wananchi kuacha kupanda miti ya mbao katika maeneo ya makazi na kusisitiza kuwa suala hilo ni lazima na siyo ombi.
Na Asukile Mwalwembe