Chama cha Wananchi CUF kimepanga kuiomba Mahakama ya Kimataifa
uhalifu ICC kuanzisha uchunguzi dhidi ya viongozi wenye dhamana
mbalimbali waliohusika kuchochea,kutoa na kusimamia maagizo yalipelekea
makosa ya uhalifu wa kibinadamu yakiwemo yanayolenga wananchi na makundi
ya watu.
Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya uvunjani wa haki ya
binadamu unaofanywa na vyoimbo vya dola dhidi ya wapinzani kwa mwaka
2015-2016, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Bw.Nassor Mazrui amesema
chama hicho baada ya kuzindua ripoti hiyo kimepanga kuchukua hatua tano
ikiwemo pia kufungua kesi katika Mahakama Kuu Tanzania dhidi ya Waziri
wa mambo ya ndani ya nchi na Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa ukiukwaji wa
haki za binadamu.
Ripoti ya uvunjaji wa haki ya binadamu unaofanywa na vyombo vya
dola dhidi ya wapinzani kwa mwaka 2015-2016,imeonyesha katika kipindi
hicho watu 300 waliwekwa rumande,watu 200 walijeruhiwa,watu 13
kudhalilishwa kijinsia ambapo watu zaidi ya 70 walivunjiwea majengo,watu
3 walipata ulemavu kutokana na matukio hayo na 40 walihama makazi yao
kukimbia vurugu za jeshi la Polisi.