Aliyekuwa mgombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
tiketi ya UKAWA kupitia Chadema na mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema
Edward Lowasa amewataka watanzania kutambua kuwa Chadema bado kipo imara
kitaendelea kuwatumikia na kwamba chama hicho hivi sasa kinajengwa
kitalam zaidi.
Mh.Edward Lowasa ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na umati
wa wapenzi wanachama mashabiki wa Chadema na watanzania wengine katika
mjiji mdogo wa Mto wa Mbu wilaya ya Monduli ambapo pia amewataka
watanzania kudumisha amani na kuwa na subira kwakuwa wakati wa utawala
wa ukombozi wa Chadema unakaribia.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Salum Mwalimu amesema watanzania
wanakila sababu ya kumshukuru Mh.Lowasa kwa utulivu aliyo uonesha baada
ya uchaguzi na kuwa Lowasa anajali utu zaidi kuliko maslahi yake na
mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Isack joseph akiahidi kutenda haki
katika utawala wa Chadema kwenye Halshauri hiyo.
Katika mkutano huo pia watu wenye ulemavu walipata nafasi ya kutoa
shukrani zao kwa wanasiasa baada ya uchaguzi mkuu wakidai panapo tokea
machafuko wao ndiyo maathirika wakubwa.