Mkuu WA MKoa WA Dar es Salaam, Mecky Said Saddick amewataka Polisi jijini hapa, kutojenga urafiki na majambazi, badala yake wahakikishe wanamaliza na kukomesha matukio yanayofanywa Mara kwa Mara na kupelekea kupoteza maisha ya watu na Mali zao.
Amesema, Polisi wahakikishe wanawatia nguvuni wote waliohusika na mauaji ya askari aliyekuwa Lindo kwenye Benki ya Access Mbagala.
Amebainisha hayo wakati wa sherehe ya kumuaga aliyekuwa Kamanda Kanda MAalum ya mkoa Dar es Salaam, Kamishna mstaafu Suleiman Kova iliyofanyika kwenye bwalo LA Polisi Oyster bay jijini Dar es salaam.