Wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kabwe, Mbeya ndiyo waliofanya vurugu kwa kuchoma matairi barabarani katika eneo hilo wakipinga hatua ya serikali kubomoa vibanda vyao.
Vibanda hivyo vilibomolewa usiku wa kuamkia leo. Wafanyabiashara walipofika Kabwe na kuona wamebomolewa, ndipo walipofanya vurugu.
Vurugu hizo zimepungua sasa baada ya Polisi kuwatawanya wafanyabiashara hao.