Hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa Njombe alifanya ziara wilayani Makete kukagua utekelezaji wa mradi wa TASAF awamu ya tatu kwa wanufaika katika vijiji kadhaa wilayani hapa
Mnyama anayeonekana kwenye picha hapo juu ni maarufu kwa jina la SIMBILISI na asilimia 90 ya wanufaika wa TASAF wamesema kuwa wanafuga wanyama hawa ambao wanazaliana kwa kasi, unakuta mtu alinunua wawili lakini ndani ya muda mfupi akajikuta anao zaidi ya kumi
Hali hiyo ilimvutia mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi na kuhamasisha wanancho wa makete wawafuge wanyama hawa na wilaya itafute soko la kuwauza kwa kuwa watahitajika sana hasa uwekezaji wa madini ya Mchuchuma na Liganga yaliyoko Ludewa ukianza wanyama hao watahitajika sana
 
 
 Posts
Posts
 
 
 
