Kesi nyingine ya CHADEMA yapigwa chini na mahakama

Mahakama kuu kanda ya Mwanza leo imefuta rasmi kesi ya madai ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa mbunge jimbo la Ilemela.
 
Kesi hiyo imefutwa kutokana na ombi maalumu la mleta shitaka Hynes Kiwia kutaka kupunguziwa gharama za kuendesha keshi hiyo jambo ambalo lilishindikana kutokana na ombi hilo  kutokidhi vigezo

Katika shauri hilo lililofunguliwa mwaka jana Hyness Kiwia aliyekuwa mbunge wa jimbo la ilemela aliwashitaki Angelina Sylivester Mabula ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo hilo.

Shauri hilo limefutwa na msajili wa mahakama kuu kanda ya mwanza Eugenia gerald na kushuhudiwa na mawakili wa pande zote mbili


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo