Simbachawene akunjua makucha yake...aagiza takataka zote zizolewa kabla ya Desemba 20

WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora George Simbachawene amewaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurungenzi wote wa halmashari nchini kuhakikisha wanazoa taka zote zilizokusanywa wakati wa siku ya uhuru kabla ya tarehe 20 mwezi huu. 
 
Kauli hiyo aliitoa wakati alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa kikao cha kumkaribisha katika ofisi ya Tamisemi mjini Dodoma. 
 
 Alisema kuwa hataki kuona hadi ifikapo tarehe 20 ya mwezi huu kuwa uchafu wa siku ya uhuru bado unaendelea kulalamikiwa na watu kuwa bado haijaondolewa katika maeneo uliokusanywa.
 
“Hadi ifikapo tarehe hiyo sitaki kusikia uchafu bado haujaondolewa katika maeneo ulipokusanywa toka siku ya uhuru lakini pia unapoondolewa huo kuna uchafu mwingine unakuja hivyo basi watendaji wanaohusika wa hakikishe kuwa wanaanda maeneo ya kuupeleka” alisema Simbachawene. 
 
 Aidha aliwataka watumishi wa Tamisemi kubadilika katika utendaji wa kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani awamu ya tano ya haitaendelea kuwalea watendaji wavivu.
 
 Kwa upande wake,Naibu Waziri wa wizara hiyo Suleiman Jaffo, aliwataka watumishi wa Tamisemi kubadilika katika utendaji wao wa zamani ili waweze kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuweza kuboresha maisha ya wananchi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo