Nauli kupanda Mbeya SUMATRA yatoa kauli nzito

Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu nchni SUMATRA Mkoa wa Mbeya imewatahadharisha wamiliki wa vyombo vya usafiri kutokupandisha nauli katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho mwa mwaka.
Afisa Mfawidhi wa SUMATRA mkoani Mbeya Denis Daudi amesema mamlaka hiyo haitasita kuwachukulia hatua watoa huduma wakiwemo wamiliki, wafanyakazi na wapiga debe wa vyombo vya usafiri watakaokiuka agizo hilo.
Akizungumza nasi, Denis amesema yamejengeka mazoeza ya kila inapofikia mwishoni mwa mwaka Mawakala wa kukatisha tiketi katika maeneo ya vituo vya maabasi, wamiliki, madereva na makondakta kulalamikiwa na abiria kwa tabia hiyo ambayo wanaifanya kwa lengo la kujiongezea kipato huku wakifahamu kuwa ni kinyume cha sheria
Taarifa iliyorushwa na Star tv ambayo haikuishia hapo imetembelea kituo cha mabasi yaendayo mikoani eneo la nane nane jijini Mbeya na kuzungumza na abiria ambao pamoja na mambo mengine wamesema tayari nauli zimepandishwa katika utaratibu ambao hawawezi kuukwepa.
SUMATRA imewataka abiria kuipa ushirikiano kwa kukataa kulipa nauli isiyoendana na hadhi ya gari na umbali wa safari husika kwa kutoa taarifa kwa Mamlaka hiyo ama kwa Askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani.
Kutokana na wingi wa abira katika kipindi hiki SUMATRA pia imewaruhusu wenye magari yanayoweza kusafirisha abiria kuyaombea kibali ili yatoe huduma.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo