Ole wako ukutwe ukiuza matunda yaliyokatwa kwenye maeneo ya wazi

Serikali imepiga marufuku wafanyabiashara wanaouza matunda yaliyokatwa na chakula katika maeneo ya wazi nchi nzima ili kuzuia mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ulioenea katika mikoa takribani 21 Tanzania Bara.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa tamko hilo la serikali na kusema ili kuumaliza ugonjwa huo ni lazima maambukizi mapya yadhibitiwe na atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.
Tamko hilo limetolewa wakati watu elfu 11,257 wakiwa wameathirika na ugonjwa huo na kati yao 177 wamepoteza maisha tangu Agost 15, mwaka huu ulipoanzia katika Mkoa wa Dar es slaam na kuenea katika mikoa 21 Tanzania Bara.
Wakati Serikali ikiwa imechukua hatua ikiwemo kuwashirikisha DAWASCO kupima sampuli za maji katika maeneo yaliyoathirika na kufukia visima 310 na vingine 98 kufungwa.

Waziri amewagia waganga wakuu wa Mikoa na wilaya kusimamia utekelezaji wa mikakati yote ya kuthibiti mlipuko huo na kuwakumbusha wananchi kuzingatia kanuni za afya.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Hamis Kigwangala ametoa maagizo ya kuteketezwa  kwa taka  zilizokusanywa siku ya uhuru na kazi ambazo zimekuwa zikizagaa mitaani.

Baada ya Mawaziri hao kuzungumza na waandishi wa habari wakatembelea katika vituo vya wagonjwa wa kipindupindu jijini Dar es salaam ambapo Waziri Ummy alipata wasaa wa kutembelea kambi ya kipindupindu iliyopo Mburahati na kujionea hali halisi ya eneo hilo pamoja na kusikiliza changamoto zilizopo huku Naibu wake akitembelea maeneo ya Buguruni.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo