Akizungumza na waandishi wa Habari kwa niaba ya serikali katika viwanja vya Ikulu Jijijini Dar es salaam katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa Rais Magufuli amaenza kazi leo hii kwa kumteua mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ni George Mcheche Masaju aliyewahi kushikilia nyadhifa hiyo, katika serikali ya awamu ya nne chini ya uongozi wa rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
Mwanasheria huyo mteule anatarajia kuapishwa kesho saa nne asubuhi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali
Aidha Balozi sefue ameeleza kuwa Rais Magufuli ameitisha Bunge la 11 ambalo litafunguliwa rasmi tarehe 17/11/2015 nakuongeza kuwa huenda mpaka kufikia tarehe 19 mwezi huu Rais atakuwa amependekeza jina la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa serikali ya awamu ya tano na kusubiri ridhaa ya wabunge.