Mkuu wa Mkoa awaagiza polisi wamkamate meneja wa kiwanda

Serikali imeliagiza Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro Kumkamata mara moja na kumfikisha Mahakamaini Meneja wa Kiwanda cha Kukoboa kahawa cha Tanganyika Coffee Curing Company LTD cha mjini Moshi Andrew Kleruu kwa tuhuma za kuhusika na upotevu  wa magunia 36 yenye uzito wa kilogramu 1764 za kahawa kutoka kwa  wanaushirika  wa chama cha G32 kilichopo mkoani humo.
Agizo la mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla likielekezwa kukamatwa kwa Meneja wa Kiwanda cha kukoboa Kahawa cha Tanganyika Coffee Curing Company Ltd Andrew Kleruu akituhumiwa kuhusika na upotevu wa magunia 36 katika ukoboaji wa kahawa kwa  msimu uliopita.
Pamoja na Mambo mengine Makala ameagiza kuchunguzwa kwa madai ya mishahara ya  wafanyakazi kiwandani hapo yanayofikia kiasi cha shilingi milioni 77.pamoja na kodi inazodaiwa na mamlaka ya mapao nchini TRA mkoani Kilimanjaro kiasi cha sh.milioni 390.
Kauli ya Makala imenilazimu kuutafuta uongozi wa chama cha G32 ili kujua ni namna gani hali hiyo imekuwa ikikatisha tamaa wakulima wa kahawa kuendelea na kilimo cha zao hili.
Tuhuma za ubadhirifu wa fedha zimeendelea kuukumba mkoa wa Kilimanjaro katika miezi ya hiv karibuni huku watumishi wa idara mbalimbali wakihusishwa na tuhuma hizo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo