Watu watano wamelazwa katika hospitali ya Mbuyula wilayani Mbinga mkoani Ruvuma baada ya kunywa togwa inayodhaniwa kuwa na sumu.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mbuyula Elisha Robert amesema wagonjwa hao ambao waliletwa hospitalini hapo wakidhaniwa kuwa wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu walibainika kuwa wamekunywa kinywaji aina ya Togwa ambacho kimesababisha waharishe.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mbuyula wilaya ya Mbinga Elisha Robati amesma aliweza kugundua kuwa homa hiyo ya kuharisha ili kuwa siyo kipindupindu baada ya kinyesi walicho toa kuwa na Rangi Nyekundu baadala ya kuwa na Rangi ya Maziwa
Wanakijiji walio ongozana na Wagonjwa hao wamesema wao wanajua kuwa mahindi yaliyo tumika kutengenezea Tongwa hiyo yalikuwa bado yana sumu iliyo tiwa ili kuyakinga Mahindi yasiharibiwe na wadudu hivyo ni bora unapo tia dawa mahindi kungoja miezi mitatu kama unavyo shauriwa na watalamu
Kamishina Msaidizi wa Police Mihayo Msekhela amethibitisha watu watano kunywa Togwa inayo sadikiwa kuwa ina sumu akiwataja kwa majina amesema ni Sitamiili Mapunda 21 Ostela Komba ambaye ni mtoto wa miezi 4 Adelina Nchimbi 20, Paulina Komba21 na Edda Kapinga 24
Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma amewaonya wananchi kuwa Makini wanapo tengeneza chakula chochote kile kuchukua tahadha ya kuhakikisha cha kula hicho hakina aina yoyote ya viashiria ambavyo vina weza kumudhu Binadamu
Hii ni Mara ya pili kwa wananchi mkoa wa Ruvuma kuathirika na kinywaji cha aina ya Togwa ambacho hutumika zaidi kukata kiu hasa yakati hizi za joto kali, mara ya kwanza watu 55 walilazwa katika hospitali ya peramiho baada ya kunywa togwa kwenye sherehe za kipaimara.