Prof. Lipumba azidi kuililia Zanzibar, atoa tahadhari

Aliyekuwa M/kiti wa  Chama cha wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba amedai kuwa M/kiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar pamoja na Tume ya  Uchaguzi ya Zanzibar- ZEC wamekiuka katiba ya Zanzibar sura ya 9 hadi 11 pamoja na Sheria ya Zanzibar ya kifungu cha 119 -hadi 129 kwa kufuta Uchaguzi uliofanyika Octoba 25 mwaka huu ambapo ametoa wito wa kufanyika mazungumzo ili kuepusha Zanzibar kutumbukia katika machafuko.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya CUF jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza tangu ajiuzulu unyekiti wa chama hicho,Prof.Lipumba amesema dosari zinazodaiwa kutokea katika Uchaguzi huo zilipaswa zielekezwe kwa ZEC na sio vyama vya siasa kwa kuwa vyama vyote vilifuata taratibu na sheria na kanuni za Uchaguzi.

Amesema kutokana na Uzoefu wake wa siasa za Zanzibar Tume ya Uchaguzi Zanzibar pamoja na wadau mbalimbali wanaoitakia mema Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wanapaswa kuelekeza nguvu zao katika mazungumzo ya kuupatia ufumbuzi mgogoro ulioibuka na sio kurudia Uchaguzi.

Aidha Prof Lipumba kuachia kuibuka kwa mgogoro huo wa kikatiba na kisiasa kunaweza kuirudisha Zanzibar nyuma pamoja na kumpa kazi rais mteule wa Tanzania kuanza kushughulikia migogoro ya kisiasa badala ya maendeleo.

Wakati huo huo Ujio wa Prof.Lipumba katika ofisi hizo kwa mara ya kwanza umewakusanya mashabiki na vijana wa CUF  katika ofisi hizo na kutoa hisia zao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo