Basi la kampuni ya Penguin lililokuwa likitoka Njombe kuelekea Bulongwa wilayani Makete mkoani Njombe limepinduka katika kijiji cha Utanziwa wilayani hapo
Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa mmoja wa shuhuda aliyekuwepo eneo la Tukio, amesema ajali hiyo bado haijafahamika vizuri chanzo chake ingawa inadhaniwa kuwa ni utelezi uliosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani hapo
Ajali hiyo imetokea leo jumapili majira ya saa 10 jioni na abiria wamepata majeraha na kupelekwa hospitali ya Bulongwa kwa matibabu zaidi na hakuna aliyefariki mpaka tunaandika taarifa hizi za awali
Taarifa zaidi utazipata kwa jinsi tutakavyokuwa tunazifuatilia
Muonekano wa basi la Penguin baada ya kupinduka
Muonekano wa basi la Penguin kwa mbele baada ya kupinduka.
Mmoja wa abiria aliyekuwa kwenye basi hilo akiwa amejeruhiwa mkononi. Picha zote na Nally Mwamba wa Eddy Blog