Mkurugenzi mtendaji wa SUMASESU Egnatio Mtawa
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Zainab Kwikwega akiwa na Makamu mwenyekiti wa bodi ya SUMASESU Reuben Mbilinyi
Wajumbe waliohuhuria uzinduzi wa mradi huo
Katibu wa TSD wilaya ya Makete Solomon Ndandu akichangia hoja katika uzinduzi huo
Mkuu wa wilaya ya Makete (aliyesimama) akizungumza na washiriki katika mradi huo
Mradi wa shule salama utakaoendeshwa na shirika la SUMASESU katika shule nne za sekondari wilayani Makete kwa ufadhili wa RFE, umezinduliwa kwa ngazi ya wilaya katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete lengo likiwa ni kupambana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanafunzi
Akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa mradi huo Mkurugunzi wa shirika la SUMASESU Bw. Egnatio Mtawa amesema mradi huo utaendeshwa katika shule nne za sekondari ambazo ni Itamba, Matamba, Mlondwe na Ikuwo pamoja na vijiji jirani vinavyozunguka shule hizo
Bw. Mtawa amezitaja changamoto kubwa walizokutana nazo wakati wa utekelezaji wa programu kama hiyo inayotekelezwa chini ya mradi wa Ujana kuwa ni pamoja na baadhi ya waalimu kukataa kutoa ushirikiano wakati wa utekelezaji, wanafunzi kukatazwa kusema ukweli dhidi ya vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa pamoja na baadhi ya kesi za vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanafunzi kuishia hewani, hali inayokatisha tamaa
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Zainab Ahmad Kwikwega amekemea kitendo kinachofanywa na baadhi ya waalimu wa shule za sekondari wanaokwamisha utekelezaji wa mradi huo kuwa kitendo hicho kinachangia kuporomoka kwa taaluma wilayani hapo na ni kinyume na sheria za nchi
Katika hatua nyingine Mkuu wa jeshi la polisi wilayani Makete SSP Rashid Lundilo ameitaka jamii kutoa ushirikiano wa kutosha pale vitendo vya ubakaji vinavyojitokeza kwa wanafunzi au mtu yeyote kukubali kutoa ushahidi mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake dhidi ya mtuhumiwa
Makamu mwenyekiti wa bodi ya shirika la SUMASESU Bw Reuben Mbilinyi amewataka wadau wote kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha utekelezaji wa mradi huo