WACHUNGAJI na vingozi wa kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Mkoani Geita wamewataka wanasiasa ambao hawakubahatika kupata nafasi ya uongozi kwenye uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni kushirikiana na wale wote walioshinda ili kuwatumikia watanzania ambao wanakiu ya kupata maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii .
Wito huo umetolewa na viongozi hao kwenye ibada maalum ya iliyofanyika katika kanisa hilo mjini Geita kumshukuru Mungu na kumuombea Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli kufuatia ridhaa aliyopata kutoka kwa wananchi wa Tanzania kupitia uchaguzi mkuu wa Octoba 25.
Wachungaji hao wamesema baada ya uchaguzi kumalizika kwa mafanikio sasa ni wakati wa kazi kwa kushirikiana na kuwatumikia watanzania wote.
Baadhi ya waumini waliohudhuria kwenye ibada hiyo wamesema wanaimani kuwa Dk. Magufuli atatimiza ahadi zake alizozitia wakati wa kampeni ili kuinua maisha ya wananchi pamoja na kuchochea kasi ya maendeleo ya taifa .
Katika ibada hiyo waumini wametumia fursa hiyo kufanya harambee kuchangia kiasi cha Milioni sita na laki tano kwa ajili ya kununua gari la kanisa hilo.