Polisi wafukuzwa kazi Kigoma kisa mitandao ya kijamii

Polisi mkoani Kigoma imewafukuza kazi askari wake watatu kwa kusambaza taarifa za uongo kupitia mitandao ya kijamii juu ya utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wa jeshi hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui amesema kutokana na utaratibu wa kijeshi, askari hao walichunguzwa na mashitaka yaliendeshwa dhidi yao kwa miezi mitatu kabla ya kuchukua uamuzi huo.


Amewataja askari waliofukuzwa kazi ni Koplo Johnson, PC Justine na WP Mercy ambao pamoja na kufukuzwa kazi, wamepewa nafasi ya kukata rufaa ikiwa hawakubaliani na hukumu waliyopewa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo