Mkuu wa wilaya atoa maagizo "magumu" kwa polisi wake

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Babati mkoani Manyara  Chrispin Meela ameliagiza jeshi la polisi kuwakamata hakimu wa mahakama ya Mwanzo kata ya Bashneti Julius Dagharo na Mwenyekiti wa kitongoji cha Birisima katika kata hiyo Rucian Labuu  kwa tuhuma za kufanya njama za kuidhulumu  familia moja shamba.
Aidha mtendaji wa kata ya Bashnet  Samwel Mtiko yeye tayari amekamatwa na amenza kuhojiwa na polisi.
Inasemekana watendaji hao, hakimu Julius Dagharo, mtendaji wa kata Samwel Mtiko na Mwkiti wa kitonjoji Rucian Labuu wameshiriki kuliuza shamba la mama Cecilia Shamle ambalo lilikuwa na mgogoro baina ya mwanamke huyo na mme wake Gidia Gwedimi.
Cecilia Shamley  anadai baada ya kudhulumiwa shamba lake la ekari moja na nusu anakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na eneo la kilimo.
Mkuu wa wilaya ya Babati Chrispi Meela katika kushughulikia kilio cha familia hiyo anapata maelezo yanayomlalamikia hakimu na mwenyekiti wa kitongo kuhusu walivyoshughulikia kesi ya chamba hilo baina ya  mama cecilina na mme wake Gwedimi.
Mkuu wa wilaya anasema serikali haiwezi kuwavumilia viongozi hao, ananza na mtendaji wa kata ya Bashnet Samwel Mtiko.
Kwa upande wa makosa ya hakimu mkuu huyo wa wilaya ambaye pia ni mwekiti wa kamati ya maadili ya mahakimu wilaya ya Babati anaiagiza polisi na TAKUKURU kushughulika.
Wananchi hao wamepongeza hatua zilizochukuliwa na serikali dhidhi ya dhuluma ya shamba kwa family hiyo ya mama Cecilia.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo