Mwanamke atimua Mbio baada ya Mwanaume aliyelala naye Kufa

Mwanaume ambaye jina lake bado halijafahamika anayedaiwa kuwa dereva wa lori amekutwa amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni 'Golden Guest House' iliyopo kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga mkoa wa Shinyanga.

Mwanaume huyo alikutwa amekufa katika chumba alichokuwa amelala usiku wa kuamkia Jumanne Novemba 14,2017.

Inaelezwa kuwa mwanaume huyo alilala katika chumba hicho na mwanamke ambaye hajafahamika jina lake ambaye alitoroka na kumuacha marehemu chumbani.


"Huyu dereva alikuwa na tingo wake,walipofika Nzega wakiendelea na safari yao,walichukua mwanamke na kuja nae Tinde,dereva alilala na mwanamke huyo na tingo alilala kwenye lori,ilipofika asubuhi ili waendelee na safari,dereva hakutokea na ndipo walipobaini kuwa amefariki dunia kwenye chumba alichokuwa amelala,lakini mwanamke huyo hakuwepo", amesema mwananchi mmoja


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo