Majambazi waua huko Tarime

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mwikwabe Mwita mkazi wa Kibasa  wilaya ya tarime mkoani Mara amefariki dunia baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi baada ya kuvamia duka ambalo marehemu alikuwa akifanya kazi ya ulinzi nyakati za usiku
 Akiongea kwa masikitika makubwa ya kuuawa kwa mlinzi wa duka lake na kuporwa mali zote zilizo kuwemo ndani ya duka hilo mmiliki wa duka, Chacha marwa  analiomba jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya lishirikiane na  raia wema ili kubaini walio tekereza mauaji ya Mwikwabe Mwita
Kwa upande wake diwani wa kata ya sabasaba Hamisi Nyanswi na na mwenyekiti wa kitongoji cha kibasa Kesewani kebacho  wamesema kwa sasa mji wa tarime hali si shwali  kutokana na kuibuka kwa vitendo vya  uvamizi wa maduka ya wafanya biashara nyakati za usiku
Kaimu mganga mfawidhi wa Hosipitali ya Halmashauri ya mji wa Tarime Asha Magore amethibitisha kupokea majeruhi mwikwabe Mwita ambae alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo