Matokeo ya uchaguzi kata mbalimbali za wilaya ya Makete

Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Luwumbu wilaya ya Makete mkoani Njombe usiku huu wa saa 06:01 amemtangaza mgombea udiwani wa CCM kuwa ni mshindi wa kata hiyo katika uchaguzi uliofanyika jana

Msimamizi huyo Bw Barton Mbedule amemtaja Mgombea wa CCM Bw Enock Ngajilo kuwa ameibuka mshindi kwa kupata kura 588 dhidi ya mgombea wa CHADEMA aliyepata kura 284

 hapa chini ni matokeo ya udiwani tu

Kata ya Ipelele, Alimivu Sanga wa CCM amepata kura 882 na Mwipelele Mbogela amepata kura 1,074, hivyo kutangazwa mshindi

Kata ya Bulongwa mgombea wa CHADEMA amepata kura 595 na Benayo Luvanda wa CCM amepata kura 793

kata ya Kipagalo Reuben Mwandilava wa CCM amepata kura 765 Alfred Nsemwa wa CHADEMA amepata kura 643

Kata ya Iwawa Baton Sanga ACT-Wazalendo amepata kura 39, Ona Nkwama wa CCM amepata kura 2,107 Asifiwe Luvanda wa CHADEMA amepata kura 2,206 na ndio aliyeibuka Mshindi

Katika kata ya Isapulano Dadiso Tweve ACT - Wazalendo amepata kura 277, Aginiwe Mahenge wa CCM amepata kura 406, na Alphonce Mbilinyi wa CHADEMA amepata kura 485

Kata ya Ukwama mgombea wa CHADEMA Vasco Chaula amepata kura 330, na mgombea wa CCM Augustino Luota amepata kura 947

Kata ya Iniho mgombea wa CHADEMA amepata kura 437 na mgombea wa CCM Jison Mbalizi amepata kura 958

Kata ya Mang'oto mgombea wa CHADEMA amepata kura 224 na mgombea wa CCM Othmund Idawa ameibuka mshindi kwa kupata kura 923

Kata ya Tandala mshindi wa udiwani ni kupitia CCM Egnatio Mtawa amepata kura 1641,dhidi ya mpinzani wake wa CHADEMA aliyepata kura Altin Sanga 'BK" aliyepata kura 416 



Kaya ya Kinyika imechukuliwa na W. Mwalyoyo wa CCM

Kata ya Kitulo imechukuliwa na mgombea wa CCM

Kata ya Lupalilo imechukuliwa na mgombea wa CCM

Kata ya Mlondwe ameshinda Alphonce wa CCM
Kata ya Matamba ameshinda mgombea wa CHADEMA
Kata ya Lupila ameshinda mgombea wa CCM Daniel Okoka
Kata ya Mbalatse ameshinda mgombea wa CHADEMA
Kata ya Ipepo ameshinda mgombea wa CCM
Kata ya Itundu ameshinda mgombea wa CCM
Kata ya Ikuwo ameshinda mgombea wa CHADEMA
Kata ya Kigala ameshinda mgombea wa CCM


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo