Mgombea urais kwa tiketi ya Tanzania Labour Party (TLP), Mhe Maximillian Lyimo apiga kura Vunjo


Mgombea urais kwa tiketi ya Tanzania Labour Party (TLP), Mhe. Maximillian Lyimo hatimaye amepiga kura yake katika Kituo cha Njia Panda, Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, baada ya mambo kuwekwa sawa. Awali Mhe. Lyimo alishindwa kupiga kura baada ya kukosekana taarifa zake kituoni hapo.

Mhe Lyimo aliyejiandikishia mkoani Dar es Salaam, jana alienda kufunga kampeni zake Jimbo la Vunjo na kulala huko. Asubuhi ya leo alienda kituo cha Njia Panda jimboni humo ili akapige kura.

Baada ya kufika kituoni hapo akiwa na kitambulisho chake cha kupigia kura, alizuiwa baada ya kukosekana fomu namba 19 ambayo kisheria inayomuwezesha mgombea urais kupiga kura ya kumchagua rais kwenye kituo chochote. Baada ya Tume ya uchaguzi kutathmini hali ilivyo na kuridhika ilimruhusu apige kura yake.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo