Viongozi wa Dini kutoka nchi 17 wakutana jijini Dar kujadili mikakati ya kumaliza VVU/UKIMWI

Na Mwandishi wetu
Viongozi wa ngazi ya juu wa dini na wawakilishi wa madhehebu ya dini kutoka nchi 17 za Mashariki na Kusini mwa Afrika wakutana Dar es Salaam, Tanzania kujadili na kuweka mikakati ya kuharakisha kumaliza maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na  Mtandao wa kimataifa wa Viongozi wa dini wanaoishi na virusi vya UKIMWI (INERELA+) pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya UKIMWI (UNAIDS) waandaa mkutano wa siku tatu wa kimataifa kujadili ushiriki wa taasisi na viongozi wa dini katika kukabiliana na maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI.
Mkutano huo ulioanza jana tarehe 02/09/2015 unafanyika katika hotel ya Kunduchi, Dar es Salaam, Tanzania na unaohudhuliwa na zaidi ya viongozi 50 wangazi ya juu wa dini na wawakirishi wamtandao wa INERELA kutoka nchi 17 za Mashariki naKusini mwa Afrika ikiwemo Tanzania.
 Wengine wanaohudhuria mkutano huo ni wawakirishi wa makundi ya vijana; wawakilishi wa mashirika ya umoja wa mataifa na wawakilishi wataasisi za serikali ikiwemoTume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania na UNESCO Tanzania.
Katika mkutano huo Mwenyekiti wa Mtandao wa Kimataifa wa viongozi wa dini waishio na VVU/UKIMWI na waliyoathiriwa na UKIMWI (INERELA+) Mch. Mpumzile Mabizela ameeleza umuhimu wa kiongozi wa dini na namna kiongozi wa dini anavyoweza kushiriki katika kutoa elimu kuhusu maambukizi ya UKIMWI, matumizi sahihi ya dawa zakupunguza makali ya VVU, unyanyapaa na namna watu wanavyoweza kujikinga na maambukizi kupitia semina mbalimbali zinazokuwa zikiendelea katika Misikiti na madhehebu mbalimbali.
Kwa upande wake Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues amewataka viongozi wa dini kujikita katika jamii kwa ajiri ya kutoa elimu inayohusu Virusi vya UKIMWI hususani kwa vijana na jamii iliyopo vijijini.
Aliongeza kuwa kutokana na sababu za kiutamaduni na mira wazazi wengi wanashindwa kuongea na watoto juu ya masuala ya jinsia, balehe na mahusiano inachangia vijana wengi kukosa elimu sahihi juu ya miili yao hususani afya ya uzazi na kujikuta wanapata matatizo ikiwemo mimba za utotoni na maambukizi ya VVU.
 Akisistiza umuhimu wa viongozi wa dini katika mapambano dhidi ya UKIMWI na mimba za utotoni, Bi. Zulmira Rodrigues aliwataka viongozi hao kushirikiki kamirifu katika kutoa elimu sahihi na kujiepusha na ushauri utakaowasaidia waamini na vijana “wakati dunia inategemea mchango wenu katika kuhakikisha watu wanazingatia matumizi sahihi ya dawa, baadhi yenu m mekuwa mkitoa elimu zinazochangia watukuacha matumizi ya dawa na hatimaye kuathiri kinga zao za mwili” alisema. Bi. Zulmira na kugusia suala la unyanyapaa na namna viongozi wa dini wanavyoweza kusaidia kupunguza“msiwatenge na kuwanyanyapaa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kwani wanahitaji elimu zaidi ili waweze kuwa katika hali ya kawaida nasi ya kiunyonge”alisema.
Naye Mwenyekitiwa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dk. Fatma Mrisho alitoa wito kwa mashirika mbalimbali kusaidiana na viongozi wa kidini katika kuhakikisha watu wana hamasika na kupima afya zao kila wakati na kusambaza elimu inayohusu maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwa maeneo mbalimbali na pia awaasa vijana ambao bado ni wadogo kutokujiingiza katika ulimwengu wa ndoa kwani vitendo hivyo vinachangia kwa kasi maambukizi mapya ya VVU.
 Kwa upande wake Dk.Warren Namara kutoka shirika la (UNAIDS),  aliongeza kuwa viongozi wa  dini ni viongozi waaminifu waadilifu na ni waelimishaji.
Kulingana na huduma yao ya kukutana na waumini kila wiki wana nafasi nzuri na pia ni rahisi sana kuweza kuwafikishia ujumbe na kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao kwa kutoa elimu ya virusi vya UKIMWI. Dk Warren alisisitiza haki ya kila mtu kupata elimu sahihi na kuwataka viongozi wa dini kutowatenga watu hasa walio kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi mfano watu wanaotumia madawa ya kulevya na watu wanaofanya biashara ya kuuza miili yao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo