Aunt Ezekiel adai amezaliwa Kisarawe, siyo CCM

STAA wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel ‘mama Cookie’ amewajia juu wanaomsema kuwa amekikacha Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kukimbilia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa hajazaliwa na chama hicho bali amezaliwa Kisarawe.

Akiendelea kucharuka, Aunt alisema kuwa hata kama huko alipo wakishindwa atakubali matokeo kwa kuwa lazima katika mchezo kuna upande utashinda na mwingine utashindwa hivyo atakubali yote.

“Ninachojua mwisho wa siku lazima kuna mshindi na mshindwa hivyo nakubali yote kwa sababu nampenda Lowassa na sijawahi kutamka kuwa mimi ni CCM kwa kuwa sijazaliwa kwenye chama hicho, nimezaliwa kijijini kwetu Kisarawe" alisema Aunt kwa jazba.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo