Rais Kikwete apewa tuzo ya kiongozi bora Afrika Mashariki

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika Mashariki kutoka katika taasisi ya East Africa Book of Records yenye makao yake makuu jijini Kampala Uganda.Pichani kiongozi wa Taasisi hiyo Dkt.Paul Bamutize akimkabidhi Rais Kikwete tuzo hiyo wakati wa hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaanm leo asubuhi.Sambamba na Tuzo hiyo Rais kikwete amepokea tuzo ya kuitambua Tanzania kama taifa bora Afrika Mashariki kwa kudumisha Amani na Utulivu,Huduma bora za jamii,na maendeleo makubwa ya kiuchumi katika kipindi cha miaka kumi
(picha na Freddy Maro)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo