Mamlaka ya mawasiliano TCRA imekanusha taarifa inayosambazwa mitandaoni hivi sasa kuwa imetuma waraka kwa jeshi la polisi kuishughulikia akaunti moja inayohusika na makosa ya mitandaoni
Taarifa hito iliyosambazwa mitandaoni ni hii hapa chini ambayo haioneshi anuani ya aliyetuma wala aliyetumiwa, tarehe, wala kumbukumbu namba, lakini pia taarifa hiyo inaonesha kusainiwa na Mkurugenzi mkuu Prof John Nkoma ambaye alishastaafu kwa mujibu wa sheria toka Juni 30 mwaka huu, na kwa sasa TCRA ina mkurugenzi mpya aitwaye Dkt Ally Simba
Taarifa hiyo Feki iliyosambazwa mitandaoni
Kufuatia usambaaji huo wa taarifa hiyo feki, mamlaka hiyo imelazimika kukanusha taarifa hiyo na kusema ni ya uongo na wametangaza kuwa watamshughulikia muhusika kwa mujibu wa sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015, na kanusho hilo limetolewa kupitia ukurasa wa twitter wa TCRA