Kushoto ni Aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi mkoa wa Njombe, Evarist Lupenza, Baada ya Kutimkia ACT-WAZALENDO Mkoani Njombe
Na Sikawa Emmanuel Sikawa
Aliyekuwa Mjumbe wabaraza kuu la Taifa jumuiya ya wazazi ccm Everist Lupenza Ametangaza rasmi leo kukihama chama cha mapinduzi CCM na kujiunga na chama cha ACT WAZALENDO kwa kile alichokiita ni kutokana na uendeshaji wa chama cha mapinduzi kuwa wa ubabaishaji.
Lupenza amesema kuwa ameamua kukihama chama cha mapinduzi kwa hiari yake mwenyewe baada ya kutafakari baada ya michakato ya kumtafuta mgombea urais pamoja na ubunge jimbo la njombe kusini.
Aidha Lupenza amesema kuwa amekuwa hapati ushirikiano toka kwa ngazi mabimbali za chama cha mapinduzi ccm kuanzia jumuiya ya wazazi hadi baraza kuu la wazazi ccm ngazi ya Taifa.
Katika hatua nyingine Lupenza ameongeza kuwa wajumbe wote wa baraza kuu la wazazi ccm taifa waliokuwa wanamuunga mkono waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa kabla hajahamia CHADEMA wametengwa na jumuiya hiyo Na kuongeza kuwa chama cha mapinduzi hakiitaji mtu muwazi hivyo ameamua kwenda kwenye chama cha kizalendo.
Amesema siasa sio mchezo mchafu kama ambavyo watu wengi wanadhani bali watu wachache ambao wanaichafua siasa na alipoulizwa kama ametoa taarifa ccm kwa maamuzi aliyofikia amesemakuwa amewatumia ujumbe viongozi wote ngazi ya mkoa na baraza la wazazi taifa lakini hadi sasa hajapewa majibu ya aina yeyote ile.
Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo la Njombe Kusini kupitia chama cha ACT WAZALENDO Emilian Msigwa Amekiri kumpokea Lupenza na kusema atawasilidha taarifa zake kwa viongozi wa chama hicho makao makuu.