Mzee anayekadiliwa kuwa na miaka sabini mkazi wa eneo la Unga limited mkoani Arusha anatuhumiwa kumfanyia vitendo vichafu mtoto mwenye umri wa miaka kumi kwa kumwingilia kimwili kwa kipindi kirefu na kumtishia kumuua endapo atatoa siri hiyo.
Mzee huyo ambaye ni baba wa kufikia wa mtoto aliyetendewa kitendo hicho anadaiwa kusababisha mtoto huyo kuacha shule na kumkabidhi majukumu mengine ya nyumbani.
Kwa mujibu wa maelezo ya majirani ni kwamba ,kabla ya kubainika kwa kitendo hicho mtoto huyo alianza kushukiwa na majirani wanaomzunguka na baadae walipombana na kutaka awaeleze kinachomsibu ndipo alipowaeleza mkasa mzima huku akimuhusisha mama yake mzazi kuwa kila alipomueleza vitendo anavyofanyiwa na baba yake huyo wa kambo mama yake hakuonesha kushtuka.
Nao majirani walioshuhudia tukio hilo wameonesha kuchukizwa na kitendo hicho huku wakimshutumu mzee kutokuwa na ushirikiano na majirani mtaani hapo na kudai kuwa mara kadhaa wamekuwa wakimuhisi kujihusisha na vitendo viovu.
blog hii ilifika katika shule ya msingi Themi anakosoma mtoto huyo na kuzungumza na mwalimu mkuu pamoja na mwalimu wake wa darasa na kudai kuwa mtoto huyo aliacha kuja shule kwa muda na walipofuatilia hawakupata majibu na hivyo kutaka kuchukua hatua zaidi ili kujua mwanafunzi huyo yupo wapi.
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa ya mount Meru Dr Idd Zuberi amesema wamekuwa wakipokea watoto wengi wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia hivyo ameitaka jamii kuwa mlinzi na kuhakikisha kuwa tabia hizo zinakomeshwa.