Hakuna cha CCM wala UKAWA: CHAUMA chaeleza matumaini ya kupata ushindi

Zikiwa zimebaki siku 29 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi cha Chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMA Hashim Rungwe ametoa tathimini yake juu ya mwenendo wa kampeni pamoja na matumaini yake katika kupata ushindi.
Rugwe amesema ingawa ziko changamoto zinazojitokeza lakini kwa ujumla kampeni zinakwenda vizuri na ana matumaini makubwa ya kuingia Ikulu kutokana na watanzania kuhitaji mabadiliko.

Akiwa Singida ambao ni mkoa wa 10 katika mwendelezo wa ziara yake ya kuwaomba Watanzania wamchague kuwa Rais, baada ya kumaliza mkutano wake Mgombea huyo wa CHAUMA Hashim Rungwe akalazimika kukutana  na waandishi wa habari kutoa tathimini juu ya mwenendo wa Kampeni na kudai kuwa wanamatumaini ya kuingia Ikulu.

Matumaini yake makubwa ni kuibuka mshindi na kuwa Rais wa Tanzania katika awamu ya tano.

Pamoja na matumaini aliyonayo, mgombea huyo anakiri kuwa mazoea na umaarufu bado ni changamoto kubwa kwani inamlazimu kutumia nguvu ya ziada kuhakikisha anatengeneza umaarufu kwa kipindi hiki na mwisho kuingia ikulu.

Hata hivyo Mgombea huyo ni mmoja wa watu wasioamini katika mafuriko ya umati kwenye mikutano ya kampeni na kusema siku ya kupiga kura ndio majibu yataonekana kwakuwa wengi wa umati wanaoupata baadhi ya wagombea ni kutokana na umaarufu na kuwashuhudia tu.

Ingawa kila mgombea wa Udiwani, Ubunge na Urais anamatumaini ya kushinda katika uchaguzi mkuu, lakini jibu la ukweli linabaki kuwa kwenye sanduku la kupigia kura siku ya Jumapili ya tarehe 25 mwezi ujao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo