Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi awaangukia wanasheria

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Jaji Damian Lubuva amewataka wanasheria kutumia taaluma yao wakati huu wa uchaguzi kuwaelimisha wanasiasa na wananchi  masuala ya kisheria yanayohusianana na uchaguzi yanayoonekana kuwatatiza ili kuwa na uchaguzi wenye amani.

Jaji Lubuva anatoa wito huo jijini Arusha kwa wanasheria wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wanachama wa chama cha wanasheria Tanganyika na kusisitiza kuwa ni vyema wanasheria wakaepuka kuwa wanaharakati.
 
Mwenyekiti huyo wa tume ya uchaguzi akatumia fursa hiyo pia kuendelea kuwatoa hofu watanzania kuhusu suala la kura kuibiwa akisistiza kuwa kura zote zitahesabiwa na kubandikwa vituoni.
 
Wanasheria hao wanakutana huku mada kuu ikiwa muskabali wa uchaguzi mkuu na jukumu la wanasheria ambapo wanasema utekelezaji wa majukumu yao utakuwa na tija iwapo wanasiasa nao watakua tayari kupokea ushauri wao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo