Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi nchini UKAWA Edward Lowasa, ameahidi kuhakikisha anapambana na tatizo la rushwa ambalo limekuwa chanzo cha umasikini nchini.
Siku 29 pekee kuelekea octobar 25 mwaka huu, sauti bado ni ile ile kila kona ya nchi akiwa mjini hai ambapo alihutubia mikutano ya hadhara katika maeneo ya Lunongai, Shirimatunda, Machame na Hai mjini Edward Lowasa amesema atahakikisha anaongoza nchi kwa misingi ya haki na usawa hukua kiahidi kutumia vema ilani ya ukawa kuhakikisha anapambana na rushwa kwani kwa muda mrefu imekuwa kikwazo kwa maendeleo ya nchi huku wachache wakinufaika na rasilimali za nchi.
Huku akionekana kujiamini kushinda katika chaguzi ujayo, Freeman Mbowe anayewania nafasi ya ubunge katika jimbo hilo la Hai amewataka wanahai na watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanafanya mabadiliko kwani ndio njia pekee ya kujikwamua na umasikini uliokithiri hasa kwa wananchi wa kipato cha chini.
Fredrick Sumaye waziri mkuu mstaafu akihutubia maelfu wakazi wa jimbo la hai amesema ni wakati muafaka wa kukiondosha chama cha CCM madarakani kwani kimeshindwa kusimamia rasilimali za nchi na kufanya nchikuendelea kuwa masikini.