Serikali yake ya awamu ya tano itakayoongozwa na Dr.John Pombe magufuli endapo itapewa ridhaa na watanzania itatoa kipaumbele na kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi ili iendelee kuimarika na kustawi bila ya vikwazo kutokana na mchango wake mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa na kupunguza ama kuondoa tatizo la ajira nchini.
Ni kauli thabiti inayoashiria utumishi uliotukuka na wenye matumaini kwa wananchi wa Tanzania inayotolewa na mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi Dr.John Pombe Magufuli mkoani Shinyanga na kutambua mchango wa sekta binafsi katika kukuza uchumi na pato la taifa pia kutoa ajira hususani kwa vijana na kuahidi kujenga serikali itakayoshirikiana
Akizungumza na mamia kwa maelfu ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga na viunga vyake katika uwanja wa CCM Kirumba mgombea huyu wa kiti cha urais kupitia CCM Dr.John Pombe Magufuli anaonesha kukerwa na wawekezaji waliobinafsishiwa viwanda bila ya kuviendeleza na mojawapo ya viwanda hivyo ni kiwanda cha nyama mkoani shinyanga.
Pia Dr.Magufuli anatoa tahadhari kwa watanzania kuhusiana hasa na viongozi wanaotumia fedha kupata madaraka kwa kuelezea madhara ya viongozi wa aina hiyo kupewa dhamana.