Mtoto achomwa moto na shangazi yake Mbinga

Mtoto Mary Emmanuel mwenye umri miaka mitano mkazi wa mtaa wa Kipika wilayani Mbinga mkoani Ruvuma amekuwa akinyanyaswa kwa kunyimwa chakula na sasa amechomwa moto kiganja cha mkono wake wa kushoto  na shangazi yake aitwaye Anneth Nyoku kwa madai ya kuiba kipande  cha nyama.

Afisa  maendeleo ya jamii wa wilaya ya mbinga mkoani Ruvuma Bi.Davina Maketa anazungumzia tukio hilo ambapo mtoto  huyo anadaiwa kunyanyaswa kwa kunyimwa chakula na kupigwa na shangazi yake anayeishi naye aitwaye Aneth Nyoku anayedaiwa kumchoma moto mtoto huyo huku wananchi wakilaani ukatili huo.
 
Naye mtuhumiwa wa ukatili huo Bi.Anneth Nyoku amesema hakuwa na nia mbaya kumchoma moto mtoto huyo bali lengo ilikuwa ni kumuonya kuacha tabia ya wizi.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma ACP Revocatus Malimi amesema taarifa za tukio hilo bado halijafika mezani kwake na atalifuatilia na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtuhumiwa huyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo