Msanii wa bongo fleva, Nay wa Mitego amemvaa mjumbe wa kamati ya Kampeni ya CCM,January Makamba na kudai yeye ni mnunuaji mkuu wa tafiti na wasanii kwa lengo la kukisaidia chama chake.
Nay alimjibu January Makamba aliyepost ujumbe ukionyesha kushangaa tuhuma dhidi ya CCM kuwa imekuwa ikinunua wanasiasa,tafiti pamoja na wasanii kwa lengo la kuulaghai umma.
"Zitto kanunuliwa. Slaa kanunuliwa. Lipumba kanunuliwa. Twaweza imenunuliwa. Synovate imenunuliwa. Wasanii wamenunuliwa. Tuwe creative kidogo" Aliandika January Makamba.
"Ni kabisaa kwani uongo? We ndo mnunuzi mkuu. Bro kama ubunifu ni hela basi we Master wa Ubunifu... @JMakamba Ongeza ubunifu bro"Alijibu Nay wa Mitego
Zitto kanunuliwa. Slaa kanunuliwa. Lipumba kanunuliwa. Twaweza imenunuliwa. Synovate imenunuliwa. Wasanii wamenunuliwa. Tuwe creative kidogo
— January Makamba (@JMakamba) September 25, 2015
@JMakamba Ni kabisaa kwani uongo? We ndo mnunuzi mkuu. Bro kama ubunifu ni hela basi we Master wa Ubunifu...@JMakamba Ongeza ubunifu bro
— MR. NAY (@naythetrueboy) September 26, 2015