Mgombea mwenza wa UKAWA amimina ahadi huko Tanga

Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA ), akiwakilisha vyama washirika vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA ),Mh.Juma Duni haji amesema iwapo watanzania watamchagua mgombea urais wa UKAWA Mh. Edward Lowassa, watahakikisha wanafufua kiwanda cha chai Lushoto, reli inayotoka Dar es Salaam kwenda Moshi kupitia Tanga pamoja na kujenga kiwanda cha kusindika juisi ya matunda ili kuwawezesha vijana kujiajiri.

Akinadi sera za Chadema na ukawa katika mikutano ya kampeni za kumuombea kura mgombea urais wa Chadema mh.Edward Lowassa ambazo zimefanyika katika majimbo ya Bumbuli,Korogwe vijijini na Korogwe mjini,mgombea mwenza huyo Mh.Juma Duni Haji akizungumzia kiwanda cha chai amesema kwamba jambo la kwanza ambalo serikali ya Chadema na ukawa italifanya pindi ikipata ridhaa ya kuingia madarakani ni kufufua kiwanda cha chai ili kiweze kutoa ajira kwa wananchi.
Mara hii jeshi la Polisi nchini ambalo kwa muda mrefu limekuwa likilalamikiwa na wapinzani kwamba linapendelea chama tawala, limekumbukwa katika ilani ya chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema ambacho kinapeperusha Bendera ya vyama vinne vnavyounda ukawa kwa askari kuhaidiwa maslahi bora ikiwa UKAWA itafanikiwa katika mbio zake za kuingia ikulu ya magogoni jijini Dar es Salaam.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo