Mgombea mwenza wa rais wa jamuhuri ya muuungano ya Tanzania kupitia CCM Samia Suluhu Hasani ameanza kampeni za kunadi sera za CCM katika mkoa wa Ruvuma kwenye wilaya za Nyasa na Mbinga huku akiwataka wananchi wa maeneo ya vijijini kupuuzia kauli za watu wanaowatisha kuwa siku ya kupiga kura kutakuwa na fujo kwakuwa zinalengo la kuwatisha wasiende kupiga kura na kuwafanya wakose haki yao ya msingi kuchagua viongozi wanaowataka.
Mh Samia Suluhu Hasani ametoa kauli hiyo katika mikutano yake aliyo ifanya katika vijiji vya Kingerikiti na Tingi wilayani Nyasa na kijiji cha maguu katika wilaya ya Mbinga ambapo alipata nafasi ya kuzungumza na wakazi wake na kuwataka wapuuzie kauli hizo kwani hakuna mtu atayeweza kumzuia mwingine kupiga kura kwakuwa tume ya uchaguzi na jeshi la polisi linajukumu ya kuwalinda wapigakura.
Akiwa katika jimbo la Nyasa mgombea ubunge katika jimbo ilo kupitia CCM mhandisi Stela Manyanya amesema yeye na madiwani wake wamejipanga kubadilisha maisha ya wakazi wa Nyasa endapo watapata nafasi ya kuchaguliwa kwani wanayatambua vizuri matatizo ya wakulima ambao ndiyo idadi kubwa ya wakazi hao.
Nao wagombea ubunge wa majimbo ya Mbinga vijijini Maritin Msuha na Sixtus Mapunda wa Mbinga mjini nao wakapata nafasi ya kunadi sera za CCM na kuainisha watakayo wafanyia wananchi endapo watafanikiwa kuingia madarakani.
