Na Gabriel Kilamlya NJOMBE
Wananchi Walionufaika na Mradi wa TASSAF Awamu ya Tatu Katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Kupitia Mpango wa Kuzinusuru Kaya Masikini Wametakiwa Kuhakikisha Fedha Wanazopata Zinawainua Kimaisha.
Kauli Hiyo Imetolewa na Mratibu wa TASAF Katika Halmashauri ya Wilaya Hiyo Bwana Cassian Nkunga Wakati Akizungumza na Kituo Hiki Ofisini Kwake Kufuatia Kuwepo Kwa Taarifa ya Zoezi Hilo Kukumbwa na Baadhi ya Changamoto Zikiwemo za Kiimani.
Bwana Nkunga Amesema Kuwa Katika Halmashauri Hiyo Walengwa Hao Ambao Wanafikia Idadi ya 4924 Kati ya 4951 Wanapaswa Kuhakikisha Wananufaika na Fedha Hizo Katika Kipindi Chote Cha Miaka kumi ya Mradi Huo Ili Waweze Kuondokana Katika Mradi Huo.
Amesema Takribani Walengwa 27 Wameshindwa Kunufaika na Mradi Huo Ambao Umegawa Shilingi 160,224,000 Kutokana na Sababu Mbalimbali Ikiwemo Kuhama Eneo Pamoja na Vifo.
Hata Hivyo Amesema Miongoni Mwa Changamoto Kubwa Zilizojitokeza Katika Zoezi Hilo ni Pamoja na Imani Potofu Huku Wengine Wakidhani Fedha Hizo ni Za Freemason na Wengine Kuwaficha Watoto.
Wakati Halmashauri Hiyo ya Wilaya ya
Njombe Ikianza Kunufaika na Mradi Huo
Hadi Sasa Lakini Halmashauri ya Mj wa Njombe Haijaanza Kunufaika Nao Kwa Kile Kinachoelezwa Umechelewa Kuingia.
Kutokana na Hali Hiyo Baadhi ya Viongozi wa Serikali za Mitaa Mbalimbali Ndani ya Halmashauri ya Mji wa Njombe Akiwemo Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mpechi Bi.Clara Mpete na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mgendela Bwana Obadia Choga Wametumia Fursa Hiyo Kuitaka Serikali Kuharakisha Mradi Huo Kutokana na Wananchi Kuendelea Kuhoji Muda wa Kufika Kwa Mradi Huo.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi