Wezi wavunja ofisi ya serikali na kuiba nyaraka muhimu


Ofisi ya Madini, Kanda ya Mashariki Dar es Salaam inautangazia Umma kwamba, usiku wa Jumapili ya kuamkia tarehe 03-08-2015 wezi walivunja Ofisi ya Madini Kanda ya Mashariki iliyopo Upanga, Dar es Salaam na kuiba vitu mbalimbali vya Ofisi vikiwemo vitabu vya Stakabadhi za malipo ya Serikali.

Katika tukio hilo, stakabadhi namba ERV 6361601-6361800na ERV 6361201, 6361202, 6361203, 6361204 ziliibwa.

Aidha, vitabu vipya vinane (8) vyenye Stakabadhi namba 6360201-6360400, 6360401-6360600, 6360601-6360800, 6360801-6361000, 6361001-6361200, 6361205-6361400, 6361401-6361600 na 6361801-6362000 viliibwa, kuharibiwa na kutupwa nje ya ofisi ya madini.

Kwa taarifa hii, tunautangazia Umma kwamba stakabadhi zote zilizoibwa na kuharibiwa hazitumiki na malipo yote yatakayofanyika kupitia stakabadhi tajwa hapo juu yatakuwa ni batili.

Tunaomba yeyote mwenye taarifa sahihi zitakazoweza kusaidia kukamatwa kwa wezi husika kutoa
taarifa katika Ofisi ya Madini au kituo chochote cha Polisi kilichopo karibu. 

Imetolewa na:
Kamishna
Msaidizi wa Madini


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo