Tamasha la Umoja Kwanza latisha mbaya Tandala wilayani Makete

 Sehemu ya Umati wa wakazi wa Tandala na maeneo ya jirani waliofika kushiriki katika tamasha la Umoja kwanza lililofanywa na Kituo cha redio cha Uplands FM cha Mkoano Njombe kwa kushirikiana na Green Fm ya Makete, kwa udhamini wa PSI Tanzania
 Baadhi ya watangazaji wa kituo cha redio Uplands Fm wakiwa jukwaani wakizungumza  na wananchi waliofia katika viwanja vya lishe Tandala (Ikonda) kushuhudia tamasha la Umoja kwanza
Baadhi ya watangazaji wa kituo cha redio Green Fm wakizungumza na wananchi waliofika kwenye viwanja vya lishe Tandala kushuhudia tamasha la umoja kwanza lililofanyia hii leo.

Vituo vya redio vilivyopo mkoani Njombe, cha 89.1 Uplands Fm kilichopo Njombe mjini na cha 91.5 Green Fm kilichopo wilayani Makete mkoani Njombe kwa pamoja vimefanya tamasha la Umoja Kwanza katika viwanja vya MTC Tandala maarufu kama lishe

Tamasha hilo lenye lengo la kutoa elimu ya kupunguza maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI pamoja na matumizi sahihi ya kondomu limedhaminiwa na PSI Tanzania ambao ni wasambazaji wa Kondomu za aina mbalimbali hapa nchini

Picha zaidi zitakujia baadaye


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo