Taarifa za matokeo ya kura za maoni Ubunge CCM Jimbo la Makete

Baada ya kura za maoni ndani ya chama cha mapinduzi CCM kwa ngazi ya Udiwani na Ubunge kufanyika hapo jana, wilayani Makete matokeo ya Ubunge bado hayajatangazwa rasmi

Kwa mujibu wa taarifa za mmoja wa kiongozi wa chama hicho wilaya ya Makete aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa madai kuwa si msemaji, matokeo hayo hayajatoka bado kutokana na kuendelea kuyakusanya hasa katika kata 7 ambapo kumeibuka utata

Hali hiyo imepelekea matokeo hayo kushindwa kutoka na mwandishi wetu bado anaendelea kufuatilia suala hili kwa ukaribu ili upate taarifa za uhakika na sahihi wa mamlaka husika

Aidha kumeendelea kuwa na mchuano mkali kati ya mbunge anayetetea nafasi yake Dkt Binilith Mahenge, na mgombea mwingine Prof Norman Sigala ambapo wamekuwa wakiongoza kwa nyakati tofauti katika matokeo ya awali kutoka kwenye kata mbalimbali

Endelea kufuatilia mtandao huu tutakujulisha


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo