Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Lindi,inawashikilia aliyekuwa mbunge wa viti maalumu mkoa wa lindi Fatuma Mikidadi na Mohamedi Utali kwa tuhumu za kutaka kutoa rushwa huku Mikidadi pia akituhumiwa kutaka kuwahonga makamanda wa TAKUKURU mkoa wa Lindi baada ya kukamatwa akitoa rushwa kwa wajumbe wa CCM jimbo la Mchinga ili wampitishe kwenye kura za maoni kugombea ubunge wa jimbo hilo.
Akizungumza na wandishi a habari ofisini kwake Kamanda waTukukuru mkoa wa Lindi,Steven Jastini Chami amesema Utali Mohamed utali ambaye ni mmoja kati ya wagombea wa jimbo la Lindi alikutwa majira saa nane usiku kata ya mbanja ,huku ndani ya gari lake kukiwa na fedha shilingi milioni nne na maboksi yaliyodhaniwa kuwa ni fedha zinazokwenda kuhonga wajumbe.
Alibainisha kuwa taarifa za kumkamata Mohamed Utaly ziliwafikia baada ya kupigiwa simu na wananchi ambao walifuatilia gari hilo.
Chami amesema fatuma mikidadi mara baada ya kukamatwa alifikishwa katika ofisi za takukuru kwa mahojiano zaidi na ndipo alipotaka kuwahonga maafisa wa takukuru kiasi cha shilingi Laki saba na alfu Themenini lakini maafisa hao walikataa na kumshilia kwa kosa jingine la kujaribu kuwahonga.
Chami amesema watuhumiwa hao wawili anasubiri ushahidi ukamilike ili hatua Zaidi ziweze kuendelea.