Dkt.Magufuli awaaga wafanyakazi wa wizara ya ujenzi

Mgombea uraisi kupitia chama cha mapinduzi Dr.John Magufuli amewaaga rasmi wafanyakazi wa wizara ya ujenzi pamoja na taasisi zinazosimamiwa na wizara hiyo huku akiwaasa kuwatumikia wananchi kw auaminifu na uadilifu pamoja kujali zaidi wananchi wa hali ya chini.

Waziri huyo wa ujenzi ameyasema hayo wilayani Arumeru mkoani Arusha wakati akizungumza na wafanyakazi pamoja na wananchi waliohudhuria mkutano huo ambapo ameitumia fursa hiyo kuwaaga rasmi wafanyakazi wanaotumika katika taasisi zilizopo chini ya wizara ya ujenzi ikiwemo Tanroads na Temesa na kuwaasa kuwa muda wake wa kuendelea kuwa waziri wa ujenzi unamalizika na kwamba chama chake cha CCM kimemteua kuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 25 mwaka huu na kuwataka wafanyakazi hao kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu na weledi na kuepuka rushwa huku akiwasisitiza kuwahudumia zaidi wananchi wa hali ya chini na wasio na sauti kwa kuwa malipo yake kama si hapa dunia basi watayapata mbinguni kwa kuwatendea vyema na haki walio wadogo.
 
Mkazi wa wilaya ya arumeru mkoani arusha ambaye pia ni mwanachama wa chama hicho aliyedai kuhudhuria mkutano wa kuwateua wagombea mkoani Dodoma Bwana.John Danielson Palangyo amemwagia sifa waziri huyo wa ujenzi kama mmoja wa viongozi waadilifu wanaopigania maendeleo ya taifa na wananchi kwa ujumla bila ya kujali ukanda,kabila wala dini na kwamba ni mpinga rushwa kwa vitendo hivyo kuteuliwa kugombea kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania ni mpango wa mungu huku akimfananisha na yusuph.
 
Dr .John Pombe magufuli amekuwa na ziara ya siku mbili mkoani manyara na arusha ambapo katika tukio la kwanza akiambatana na makamu wa rais dr mohamd gharib bilal wameweka jiwe la msingi wa ujenzi wa barabara ya kia mererani pamoja na kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya njia nne mkoani Arusha.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo